Kuna maeneo ambayo hayana barabara kabisa, Je, maeneo hayo yataingia kwenye mradi huu wa urasimishaji?
Majibu: Zoezi hili la urasimishaji lina lenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za jamii kama barabara, soko, makaburi na zahanati ili kutengeneza maeneo yenye miudombinu ya kijamii. Hivyo maeneo yasiyo na barabara yanaruhusiwa kuingia kwenye mradi ili barabara zipatikane.

Kuna watu walipimiwa maeneo yao kama mashamba na wakauza viwanja ndani ya maeneo hayo, Je mradi huu wa Kupanga na Kupima utawahusu na wao?
Majibu: Kwa wakazi waliopima maeneo Yao Kama mashamba chini ya sheria ya Ardhi namba 5, 1999 upimaji huo utafutwa Na watapimiwa upya maeneo hayo ya viwanja Kama inavyoelekeza katika sheria ya Ardhi namba 4, 1999.

Kuna watu tumewekewa mawe ila hatujapata hati miliki ya maeneo yetu, Je mradi huu utahusisha huduma ya kupata hati miliki ya maeneo yetu?
Majibu:Kwa wakazi waliopima maeneo na taarifa zao ni sahihi ila hawana hati miliki za maeneo yao, wataingia katika mradi huu katika hatua ya kumilikishwa maeneo yao.

Ni hatua ipi mtaonyesha viwanja vya wananchi vilivyo katika maeneo ya huduma za kijamii kama maeneo ya wazi, masoko n.k?
Majibu:Katika hatua ya kwanza kabisa ya mradi ambayo ni UTAMBUZI wananchi watapata fursa ya kutambua matumizi yaliyo katika maeneo yao kama ilivyoainishwa katika ramani za Mipango miji iliyopo. Pia miundombinu muhimu kama umeme mkubwa na barabara kubwa itaainishwa katika hatua ya utambuzi.

Kwa maeneo yenye migogoro ya Ardhi, Je mtachukua hatua gani ili kuhakikisha mradi unafanikiwa?
Majibu:Kwa maeneo yote yenye migogoro ambayo imetatuliwa na haijafika mahakamani yanafursa ya kuingia kwenye mradi iwapo migogoro yake itatatuliwa, lakini kwa maeneo yote ambayo migogoro yake ipo mahakamani hayataruhusiwa kuingia kwenye mradi. Je, viwanja vikubwa vinatakiwa kuwa na wa ukubwa gani kutokana na sheria za Mipango Miji? -Kutokana na viwango vya Mipango Miji kiwanja chenye ujazo wa mdogo ni mita za mraba 2000. . Kwa wakazi ambao hawana uwezo kabisa mnaweka utaratibu gani wa kuwasaidia ili wapate huduma hii ya Kupanga na Kupima? -Kwa wananchi ambao wataidhinishwa na Mtaalamu wa kijamii kutoka kampuni ya HUSEA kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya mtaa pamoja na Kamati ya wawakilishi wa wananchi watapangiwa na kupimiwa bure.